Pages

Wednesday, 26 June 2013

MWANAMUZIKI DEMINGONGO LUCIEN KUKAMILISHA ALBUM YAKE YA NNE

Kukokana na kuzamia nchini paris kwa muda wa miaka 26 Luciana Demingongo sasa ameamua kutoa album yake ya nne ambapo ni album ambayo ipo nje ya band yake ambayo anaitumikia kwa sasa ya zimpompa pompa band

Demingongo ambae amewahi kuimba band mbalimbali nchini Congo ambapo aneimba na moja ya wanamuziki kama vile Awilo Longomba ambapo kipindi hicho alikuwa ni mpiga gitaa yeye  akiwa muimbaji walifanya kazi nyingi sana mpaka awilo kuhamia uimbaji

Demigongo amesema hivi karibuni anatarajia kuja DRC kusalimia na ameweza kutaja album ambazo anazo mpaka sasa ambapo album yake ya kwanza aliitoa mwaka 2012 iliyofahamika kama DEMINGONGO ZANZIBAR ambayo inanyimbo 9 moja wapo ni,Tempo,resistance,Rokia,Chanteau Rouge,Ange Volcan,Adisha,Zanzibar na Et poutant

A lbum yake ya pili inafahamika kama LUCIANA DEMINGONGO ANGE VOLICAN na album yake ya tatu inafahamika kama LUCIANA DEMINGONGO ROKIA.

Demingongo amesema album yake ya nne ni album ambayo itakuwa ya kuotea mbali zaidi kwani amejipanga zaidi na ameifanya kwa umakini wa hali ya juu za na hivyo amewaomba mashabiki wote wote wa muziki wa dance Congo na Tanzania kusikiliza nyimbo mbalimbali ili kupata jumbe ambazo zinapatikana katika nyimbo hizo
                                                                AFRIQUE MOTO PAMOJA

Sunday, 23 June 2013

BAADA YA KUSAMBARATIKA KWA WANAMUZIKI WA BAND YA TEN BROTHERS SASA KUJA KIVINGINE

Band ya Ten Brothers band kutoka Mkoani Dododma kwa sasa wamejipanga upya mara baada ya kutoka katika wwakati mgumu wa kusambaratika kwa wanamuzi mbalimbali ambao walikuwa katika band hiyo

Kiongozi wa band ya Ten brothers Bwana Juma Kibonge amesema kuondoka kwa aliekuwa manager wa band hiyo pamoja na baadhi ya wanamuziki hakuja athiri kitu chochote katika band yake na anaamini kuwa mpaka sasa watafanya vizuri katika muziki huu wa dance mkoani hum
Bwana Kibonge amesema mpaka sasa kuna nyimbo nyingi mpya ambazo ziko tayari na ni nzuri zaidi achilia mbali na nyimbo ya nyumbani ni yumbani na nyingine nyingi za zamani

Kibonge amesema kwasasa wanamuziki wapya ambao wanfanya kazi yake vizuri na kwa sasa wanamadancer wa kike watatu ambao wamesajiliwa jana katika band hiyo
                                             BURUDIKA NA AFRICA MOTO.

MKALI WA DRUMS NCHINI MARTIN KIBOSHO KUNGA'RA ZAIDI NCHINI INDONESIA

Mkali wa drums nchini tanzania ambae anaitumikia bandi ya Extra bongo chini ya uongozi wake Ally Choki ameonekana kuwa nyota zaidi katika upigaji wake wa kazi hapa nchini kwa sasa yupo Indosesia kikazi amesema anatarajia kurudi nchini hivi karibuni mara baada ya kumaliza ziara yake nchini humo
Martini kKibosho ambae alienda kikazi ambapo mara nyingi hufanya kazi na band ya morther Africa ambayo humchukua kila mwaka kutokana na kukubali kazi yake
Kibosho amesema onyesho hilo hua ni la kimataifa ambapo hufanyika nyichi mbali mbali ambapo kwa sasa yupo na wanamuziki wa nchi mbalimbali kwa ajili ya onyesho hilo amesema anamshukuru mungu mpaka hapo alipo kwa sasa na kuwashukuru uongozi wa band yake ya extra bongo
Kibosho amesema toka ameondoka nchini anamiezi mitatu mpaka sasa na anatarajia kurudi nchini Tanzania mwezi wa nane ili kuendelea kuitumikia band yake ya Extra bongo
namshukuru sana raisi wa band ynagu ya Extra Bongo Ally Choki kwa kuwa pamoja nami bega kwa bega kwa kunisapport mpaka leo hii amezungumza Martin Kibosho akipokuwa akizungumza leo mapema na Queen Jozzee wasafu ya AFRIQUE MOTO.Ukiona hii like blog hii ili tucheze wote.
                                                    TUCHEZE AFRICA MOTO PAMOJAA.

Saturday, 22 June 2013

MWANAMUZIKI MUKONGWE WA DANCE DEKULA KAHANGA YUPO MBIONI KUTOA ALBUM YAKE MPYA

Dekula Kahanga ambae ni mkongwe wa muziki huu wa dance ambae kwa sasa makazi yake ni makubwa ni Nchini Swedeni kwasasa amesema mpaka leo hii ananyimbo sita ambazo zipo tayari na bado anaendelea kurekodi nyimbo nyingine ambazo zitakamilisha album yake ambayo inatarajia kuwa na  nyimbo kumi .
Dekula ambae ni mmiliki wa band ya DEKULA BAND ambapo makazi yake ni stockhom, mwimbaji,mtunzi,na mpiga gitaa amesema mpaka sasa nyimbo ambzo zipo tayari ni pamoja na mshog remix,ammy,amani,dunia kuna mambo,bombalaka na ngoma ya kilo na dkeula amesema mpaka sasa bado hajaanza kuruhu nyimbo zake kupigwa kwenye media yeyote mpaka atakapo kamilisha album yake
                                                       CHEZA NA AFRICA MOTO

BAADA YA KUTOKA EXTRA BONGO RAMA NA KUHAMIA TWANGA PEPETA PENTAGO AMJIPANGA UPYA

Baada ya kuitumikia band ya extra bongo kwa muda mrefu mwanamuziki Rama Pentagon na kuhamia band ya The African stars wana wa kutwanga na kupepeta Pentagon amesema kwa sasa amejipanga upya kwa ajili ya kuimarisha kipaji chake ambapo kila mutu anajua kuwa Rama anamchango gani katika game la muziki wa muziki nchini
pentagoni ni miongoni mwa wanamuzi ambao wameonekana kuwa nyota ya muziki huu wa dance kwa muda murefu hapa nchini tanznia
pentagoni alihamia twanga mara baada ya kufanya kazi kwa muda mrefu katika band ya Extra Bongo chini ya uongozi wake Mzee wa farasi Le Kamarade Ally Choki.
Pentagoni amesema hayo aliokuwa akizungumza na safu ya   Africa Moto baada ya kuingia katika band ya Twanga  pepeta amesema kwa sasa yupo mbioni kutoa nyimbo zake mbili matata ambazo zitafanya vizuri katika muziki huu kwa sasa yupo katika mazoezi ambapo twanga pepeta wanrajia kuzindua album yao ya nyumbani ni nyumbani Pentagon amesema nyimbo ambazo atazitoa ni thamani ya mtu na jirasi 
Pentagoni amewashukuru sana mashabiki wote ambao wamempokea vizuri baada ya kutua twanga pepeta
                                TCHEZE PAMOJA AFRICA MOTO NA QUEEN JOZZEE

BAND YA AKUDO IMPACT KUPIGA SHOO YA NGUVU JIJINI MWANZA

Baada ya kupiga shoo matata mkoani dodoma vijana wa masauti akudo impact walielekea mwanaza jana walipiga shoo nyingine geita leo 22 06 2013 wanapiga Mwanza jokes live pub Pasians ambapo watasindikizwa na wanamuziki wa kizazi kipya ambao watamili jukwaa vizuri kabisa  atakuwepo Hussein Machozi na Baba Levo kwa kiingilio cha shiling elfukumi tu
Baada ya shoo hiyo watapiga Kahama 23 06 2013 masabo picnic Center kwa kiingilio cha tsh 10000 wakiwa na baba Levo na Hussein Machozi,tarehe 24 06 2013 watakuwa Shinyanga kakola sambamba na wanamuziki wao tarehe 26 06 2013 watakuwa Tabora FrankMan Palace kwa kiingilio cha sh 15,000 huku wakisindikizwa na mwanamama mwimbaji wa taarabu ambae pia ni dada yake mzee Yusuph  Khadija Yusuph,Baba Levo na Hussein Machozi tarehe 27 06 2013 watakuwa Kaliua Millenium Hall kwa kiingilio cha sh 5,000 tarehe 29 06 2013 watapiga Kigoma Kibo Peak Hall kwa ts 10000 bila kumsahau khadija yusuph shuhuadia shoo matatakutoka kwa vijana wa masauti

BAND YA TNC CONECTION WATOTO WA MAKAO IMEONGEZA WANAMUZIKI WAPYA

Band ya TNC Conection watoto wa makao wamejipanga upya na kuongeza wanamuziki wengine katika band yao
wanamuziki walioongezwa katika band hiyo ni mpiga gitaa mmoja na mwimbaji mmoja ambae alikuwa rikizo kwa sasa amerejea kundini baada ya kukaa kwa muda mferu mpiga gitaa huyo anajulikana  kwa jina la God na mwimbwji anaejulikana kwa jija la Lucy wameamua kutumikia band hiyo baada ya kuona ni band ambayo inamalengo makubwa
Awali band hiyo ilikuwa katika maandalizi ya kutoa album yao mpya ambapo ilikuwa katika hatua za mwiisho kumalizima lakini kwa sasa kutokanan na kukosekana kwa fedha na wadhamini imekwama mpaka watakapo pata fedha na kuomba kama kuna mtu anahitaji kudhamini band hiyo ni vyema akajitokeza

kama wewe ni mpenzi wa burudani hizi usikose kushuhudia shoo yao leo whitecorner nkuhungu kutoka tnc conectio watoto wa makao habari ndio hiyo.

RAISI WA WENGE MUSICA MASON MERE WERRASON ACHAGULIWA KUWA BALOZI WA AMANI KWA NCHI ZA AFRICA

Raisi huyo ambae pia ni mmiliki wa band ya Wenge Maison Mere ameteuliwa kuwa balozi  wa afrika kwa ajili ya kushughulikia  maswala ya watoto askari barani humo


sherehe hiyo ilifanyika kinshasa amabpo ilihudhuliwa na viongozi mbalimbali wa africa ili kumuunga mkono mwanamuziki huyo ambae ndio balozi,na baadhi ya viongozi waliohudhuria ni kutoka UNESCO,UN na wakisindikizwa na waziri wa utamaduni wa CONGO DRC
Baada ya uteuzi huo kuna party ambazo zimeandaliwa kwa ajili ya mwanamuziki huyo ambapo zitafanyika huko Drc
Werrason aliongozana na wanamuziki wa band yake nao pia wamesema kuwa wamefurahishwa sana na uongozi wa kiongozi wao kwani wanaona jinsi gani ambavyo raisi wao amekuwa akijituma kwa bidii katika kufanikisha mambo mbalimbali
Kwa muda mrefu sasa Werrason ni nyota ambae ameng'ara katika muziki wa dance barani affrica na hata duniani nzima kwa ujumla kumbuka kwamba werrason ni kati ya waanzilishi wa wenge musica BCBG 4*4 kipindi inaanzishwa
MERCI

Friday, 21 June 2013

HATIMAYE RAISI WA AKUDO CHRISTIAN BELLA KUTUA NCHINI BAADA YA KUONDOKA KWA MUDA MREFU

Raisi wa band ya Akudo Impact Chrisitian Bella amerejea nchini baada ya kukaa kimya kwa muda mrefu nchini sweden ambapo alienda kikazi ,Chrisitian Bella amerejea na kwa sasa atafanya kazi na band ya Diamond sound Original chini ya uongozi w Liva

baada ya kuzungumza na Liva  katika safu ya Africa moto ambae ni raisi ya band ya Diamond amesema kwa sasa diamond imemchukua  Belaa kwa ajiri ya kufanya nae shoo tano ambazo zinatarajia kufanyika
LIva amesema mbali na christiani bella imemchukua pia Ndanda cCossovo ambae ampapo imeshamsajili katika bandi ya diamond sound origina
Liva amesema Christian Bella hajatoa kauli yake kuwa atafanya na band gani kati ya akudo na diamond