Pages

Thursday, 1 September 2016

KUPATWA KWA JUA TANZANIA



Tukio la kupatwa kwa jua limetokea leo katika Kijiji cha Rujewa Wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya, Katibu wa Mila wa katika kijiji hicho Mwanasimtwa Mwagongo amesema tukio hilo  ni ishara ya Mwenyezi Mungu kuukubali uongozi wa Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais John Magufuli.

Hii itakuwa ni mara ya kwanza Tanzania kutokea tukio hilo tangu Aprili 18, 1977 na tukio kama hilo la kihistoria linatarajiwa kutokea tena nchini Mei 21, 2031.


Mbali ya Rujewa ambako watu wameona tukio hili la kupatwa kwa jua kwa asilimia 97 sawa na miji ya Makambako, Masasi, Mbeya, Tunduru, Njombe na Sumbawanga, miji mingine ambayo imeona tukio hilo kwa ukaribu zaidi wa asilimia 96 ni Katavi, Nachingwea na Songea ikifuatiwa na Kigoma, Iringa, Mtwara na Lindi.
Akizungumza   na waandishi habari za Utalii na Uwekezaji Tanzania (TAJATI) nyumbani kwake katika Kata ya Isisi, Mwagongo amesema tukio hilo la kupatwa kwa jua nchini si mkosi, bali ni sawa na taa iliyokuwa imezimika na sasa imewashwa na kuongeza kuwa, ni ishara kuwa Mungu ameukubali utawala uliopo madarakani na ndiyo sababu ametoa giza na kuleta nuru.

Amewaasa viongozi wa dini zote kote nchini kuliombea tukio hilo ili lifanyike na kupita kwa amani na pasiwepo na uvunjifu wa amani utakaosababisha jamii kutoa tafsiri ya tofauti baada ya tukio hili la kihistoria ambalo limefanyika kati ya saa 4.15 asubuhi hadi saa 8.00 mchana.


baada ya tukio hilo, wazee wa kimila watachinja ng’ombe kwa ajili ya kumshukuru Mungu kwa neema ya tukio hilo na pia kumwomba aiepushe jamii na madhara yoyote yanayoweza kujitokeza.


Hapo zamani watoto walikuwa hawaruhusiwi kutoka nje siku ya tukio hili. Wazee waliamini ni ajali ya kugongana jua na mwezi na wanaoumia ni wanadamu hasa watoto kwa kusababishiwa milipuko ya magonjwa mbalimbali


Lakini kwa sasa tunatambua kuwa ni tukio la kisayansi na kutokea kwenye eneo letu ni neema kutoka kwa Mungu. Kupitia tukio hili dunia itaijua Tanzania, itaijua Mbarali na itaijua Rujewa. Ni tukio ambalo limetutangaza.



Monday, 29 August 2016

MKUTANO WA 36 WA NCHI ZA SADC KUFANYIKA LEO HUKO SWAZILAND



Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe SAMIA SULUHU HASSAN amewasili mjini Mbabane - Swaziland leo kwa ajili ya kuhudhuria mkutano wa 36 wa Wakuu wa nchi na serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika- SADC. 

Makamu wa Rais SAMIA SULUHU HASSAN atamwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano Tanzania Dakta JOHN MAGUFULI katika mkutano huo ambao unatarajia kufanyika leo tarehe 29 Agosti 2016 ambapo Tanzania inatarajiwa kukabidhiwa nafasi ya Uenyekiti wa Jumuiya hiyo.

Mkutano huo wa 36 wa SADC ni maalum kwa wakuu wa nchi na serikali wanaounda Kamati ya siasa, Ulinzi na usalama ambao watajadili kwa kina hali ya siasa na usalama, demokrasia na maombi ya Burundi na Comoro kwa ajili ya kujiunga na SADC.

Makamu wa Rais Mhe, SAMIA SULUHU HASSAN katika msafara wake ameongozana na Waziri wa Mambo ya nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa Augustine Mahiga, Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji John Mwijage na Waziri wa Biashara, Viwanda na Masoko wa serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Amina Salum Ali.
 

Tuesday, 26 July 2016

SIKUKUU YA MASHUJAA YAFANYIKA KITAIFA MKONI DODOMA

TAZAMA PICHA ZA SIKUKUU YA MASHUJAA ILIYOFANYIKA KITAIFA MKONI DODOMA NA KUHUDHURIWA NA VIONGOZI MBALIMBALI.




























Friday, 13 May 2016

HRW NA AMNESTY ZAITAKA UGANDA KUMKAMATA AL-BASHIR

 
  
 Mashirika ya kimataifa ya kutetea haki za binadamu yameitaka serikali ya Uganda kumkamata Rais Omar al-Bashir wa Sudan na kumkabidhi kwa Mahakama ya Kimataifa ya Jinai ICC, kwa tuhuma za mauaji ya kimbari katika eneo la Darfur na jinai dhidi ya binadamu. 
Mashirika ya kutetea haki za binadamu ya Amnesty International na Human Rights Watch yameitaka serikali ya Uganda kutekeleza wajibu wake wa kimataifa na kumkabidhi kwa mahakama ya ICC, Rais wa Sudan ambaye alienda mjini Kampala kuhudhuria hafla ya kuapishwa Rais Yoweri Museveni. 

Muthoni Wanyeki, Mkurugenzi wa Amnesty International katika kanda ya Afrika Mashariki, Pembe ya Afrika na eneo la Maziwa Makuu amesema Uganda ni mwanachama wa Mkataba wa Roma uliobuni Mahakama ya Kimataifa ya Jinai ICC na hivyo, iwapo itafeli kumkabidhi Rais wa Sudan, itakuwa imeshindwa kutekeleza wajibu wake wa kimataifa. Hii ni katika hali ambayo, baada ya kula kiapo hapo jana, Rais Museveni aliikashifu ICC na kusema kuwa mahakama hiyo imegeuka na kuwa chombo cha kuwadhalilisha viongozi wa Kiafrika huku ikiwasaza viongozi makatili wa nchi za Magharibi

. Kauli ya Museveni iliwaghadhabisha wajumbe wa Marekani na Umoja wa Ulaya waliokuwa wamehudhuria sherehe za kuapishwa kwake katika Viwanja vya Kololo jijini Kampala na kuwafanya kuondoka kwenye hafla hiyo. 

Itakumbukwa kuwa, serikali ya Afrika Kusini ilikataa kumkamata Rais Omar al-Bashir ambaye alishiriki mkutano wa viongozi wa Afrika uliofanyika mjini Johannesburg Julai mwaka jana. 

Aidha Kenya ilipuuza wito wa kumkamata na kumkabidhi kiongozi huyo kwa Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai ICC anakotakiwa kujibu tuhuma za mauaji ya kimbari katika eneo la Darfur na jinai dhidi ya binadamu; alipohudhuria sherehe za kuapishwa Rais Uhuru Kenyatta wa nchi hiyo ya Afrika Mashariki mwaka 2013.

RAISI MAGUFULI ATAKA WATU WALIOUWA WATU SABA WA FAMILIA MOJA WAKAMATWE MARA MOJA

  
Rais   wa jamhuri ya muungano wa Tanzania  Dk. John Magufuli amesikitishwa na mauaji ya kinyama yaliyotokea hivi karibuni baada ya  watu saba wa familia moja waliokatwa mapanga katika Kijiji cha Sima wilayani Sengerema mkoani Mwanza.

kutokana na tukio hilo kutokea  Rais Magufuli ameviagiza vyombo vya dola kuwasaka kwa nguvu zote, watu waliohusika na mauaji hayo na kuhakikisha wanatiwa mbaroni hara iwezekanavyo.

Akitoa salamu za pole nyumbani kwa wafiwa  Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan, amesema Rais Magufuli ameguswa na tukio hilo 



makamu wa raisi amesema Rais Magufuli ametaka wahusika wote wakamatwe ndani ya kipindi kifupi, kwa sababu mauaji ya aina hiyo hayakubaliki hata kidogo na hawezi kuvumilia katika nchi yake.

WAZIRI WA HABARI, UTAMADUNI, SANAA NA MICHEZO Mh. NAPE NNAUYE ASOMA BAJETI YA WIZARA YAKE BUNGENI DODOMA

   Waziri wa Habari, Utamaduni, sanaa na Michezi Mh. Nape Nnauye amewasilisha bungeni makadilio ya mapato na matumizi ya fedha kwa mwaka 2061/2017 kwa wizara hiyo na kusema sekta ya maendeleo ya sanaa imefanikiwa kwa mwaka 2016 kwa kufanikiwa kwa wasanii wawili nchini kushinda tuzo za African Magic Viewers Choice Awards - AMVCA 2016 HUKO Nigeria.

   Wasanii hao ni Bw. Single Mtambalike (Richie) Filamu ya Kitendawili kipengele cha filamu bora ya lugha ya asili(Kiswahili) na Bi. Elizabeth Michael (Lulu) Filamu ya Mapenzi ya mungu kipengele cha Filamu bora Afrika Mashariki.

   Vilevile Mh. Nape amesema muongozaji wa filamu ya "Dogo Masai" Bw. Timoth Cornad alipata tuzo ya Calfonia Viewers Choice Awards huko marekani. Kwa upande wa muziki wasanii wanne walipata tuzo mbalimbali nje ya nchi.

   Jumla ya tuzo 20 zimepatikana kutoka kwa wasanii wafuatao; Bw. Nassib Abdul (Diamond) tuzo 17, Bi. Vanessa Mdee tuzo 1, Bw. Malima Mayunga tuzo 1 na Bw. Omary Nyembe (Ommy Dimpoz) tuzo 1.

   Aidha Mh. Nape amesema Wizara kwa kushirikiana na wadau wa sanaa ilifanikisha wasanii nchini kupata tuzo za sanaa kwa mwaka 2015/2016. Tuzo zilizotolewa ni "Tanzania Kilimanjaro Music Awards" - 34, Tuzo za siku ya Msanii - 4 na Tuzo za watu 13.

  Waziri wa Habari, Utamaduni, sanaa na Michezi Mh. Nape Nnauye akiwasilisha   Bungeni Makadilio ya mapato na matumizi ya Fedha kwa mwaka 2016/2017.



    Mbunge wa Mbeya Mjini Mh. Joseph Mbilinyi - SUGU akitoa hotuba ya kambi rasmi ya    upinzani kuhusu makadilio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ambaye pia ni waziri kivuli wa wizara hiyo.

   Akitoa hotuba kwa kambi rasmi ya upinzani Mh. Joseph Mbilinyi amewashukuru wananchi wa mbeya mjini kwa kumchagua na kufanikiwa kuwa msanii wa kwanza wa Hip Hop duniani kuwa Mbunge na kumtaja aliyefuata kuwa ni Mh. Joseph Haule - Prof. Jay.

 

 Msanii wa Filamu nchini Wema sepetu akifuatilia kwa makini hotuba ya Mh. Nape bungeni Dodoma.

 

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mh. Nape Nnauye akiwa katika picha ya paomja na wasanii mbalimbali waliokuwepo bungeni wakati akiwasilisha makadilio ya mapato na matumizi ya wizara yake.


Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mh. Nape Nnauye akiwa katika picha ya pomoja na mabloger mbalimbali mbele ya lango kuu la bunge.


Msanii wa Filamu JB akiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi wa shule ya sekondari ya Magubike iliyopo Mkoani Morogoro waliokuja bungeni kujifunza namna ya bunge linavyoendeshwa.


Msanii Richi Richi na JB wakiwa katika picha na wadau wa Filamu bungeni Mjini Dodoma walikuja kusikiliza hotuba ya Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo iliyowasilishwa leo Bungeni.

 

Thursday, 12 May 2016

DIAMOND NA MAFIKIZOLO NDANI YA MJENGO WA BUNGE

    Bunge la Tanzania Mkutano wa 3 kikao cha 18

    Diamond na Mafikizolo wakiwa VIP Bungeni baada ya kualikwa na Waziri wa Habari,    
    Sanaa na  Michezo Mh. Nape Nauye.
    Diamond, Mafikizolo na Waziri wa Habari, Sanaa na Michezo Mh. Nape Nauye pamoja na   
    Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira Mh. January Makamba
    kwenye picha ya pamoja mbele ya lango kuu la bunge.

   Diamond akiwa na wapenzi mbalimbali wa burudani pamoja na wabunge katika picha ya  
    pamoja mbele ya lango kuu la bunge.


INTERVIEW YA MAFIKIZOLO NA WAANDISHI WA HABARI BUNGENI MJINI DODOMA KBLA YA KUFANYA SHOW UDOM.





PIA NAE DIAMOND ALISEMA HAYA ANGALIA INTERVIEW YAKE HAPA CHINI


Friday, 11 March 2016

JESHI LA POLISI MKOA WA DODOMA LIMEFANYA MSAKO NA KUKAMATA SILAHA 26 AINA YA GOBORE NA MITAMBO YAKE

Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma limefanya Operesheni na Msako mkali katika Wilaya zake zote na kukamata makosa mbalimbali. Operesheni hiyo ilianza kufanyika tarehe 22/02/2016 hadi 06/03/2016.

Akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Kamishna Msadizi wa Polisi LAZARO MAMBOSASA – ACP amesema katika Operesheni hiyo jumla ya silaha haramu 19 aina ya Gobore zimesalimishwa na silaha saba (7) zimekamatwa za watu waliokaidi utii wa sheria, mitambo miwili ya kutengeneze silaha hizo haramu imekamatwa pamoja na watuhumiwa saba.

Kamanda MAMBOSASA amesema watuhumiwa wote ni wakazi wa kijiji cha MANDA Tarafa ya MPWAYUNGU Wilaya ya Chamwino Mkoa wa Dodoma  na wamekuwa wakimiliki silaha hizo kinyume cha sheria  na wakizitumia katika uhalifu mbalimbali hasa uwindaji haramu katika hifadhi ya RUAHA inayopakana na mkoa wa Iringa.

Aidha Kamanda MAMBOSASA amesema kutokana na operesheni hiyo watu 19 waliweza kusalimisha silaha zao katika ofisi za serikali za vijiji na hawakuchukuliwa hatua kwa kuwa walitii sheria bila shuruti.

Vilevile Kamanda MAMBOSASA amesema katika Wilaya za Dodoma, Kondoa na Kongwa walikamatwa watuhumiwa 32 wa makosa ya Kupatikana na Bhangi, jumla ya misokoto misokoto 672 ilikamatwa.  Watuhumiwa 11 walikamatwa kwa kosa la Kupatina na Pombe haramu ya Moshi na jumla ya lita 260 zilikamatwa.  Watuhumiwa 7 walikamatwa kwa kosa la Kupatikana na madawa ya kulevya aina ya Mirungi Kilogram 43.

Pia Operesheni ilihusisha makosa ya Usalama barabarani na kukamatwa kwa jumla ya pikipiki 265 kwa makosa mbalimbali, ambapo pikipiki 241 zilitozwa faini na kiasi cha fedha Tsh. 7,230,000/= zilipatikana kutokana na tozo. 

Kamanda MAMBOSASA ametoa wito kuwa msako mkali unaendelea na watu wote wanaomiliki silaha haramu kinyume cha Sheria wasalimishe silaha hizo kwa hiari kwenye  Ofisi za Serikali na vituo vya Polisi mapema iwezekanavyo na hawatachukuliwa hatua.  Wale wote wanaomiliki silaha kinyume cha Sheria wasiotayari kusalimisha wafichuliwe ili wachukuliwe hatua za kisheria dhidi ya umiliki haramu wa silaha. Aidha wananchi waache kujihusisha na vitendo vya uhalifu wa aina yoyote na kufanya kazi halali kujipatia kipato halali kwa familia zao kwani msako utakuwa endelevu wasije wakaishia jela na kuziacha familia zao zikiteseka.

Katika matukio mengine Kamanda MAMBOSASA amesema mnamo tarehe 07.03.2016 majira ya saa 16:00 huko katika Hospitali ya Mkoa wa Dodoma mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la BASILI MSABILA mwenye miaka 24, Mwanafunzi wa Chuo cha Serikali za Mitaa - HOMBOLO Dodoma ngazi ya cheti, alifariki dunia wakati anatibiwa baada ya kujeruhiwa kichwani kwa chuma na Mwanafunzi mwenzake aitwaye CHARLES MAKELE, miaka 19, mwenye miaka 19 mwanafunzi ngazi ya cheti kozi ya utawala chuo cha TAMISEMI Hombolo. 

Uchunguzi wa awali unaonesha kuwa chanzo cha tukio hilo ni ugomvi wa kugombania chaja ya simu mali ya marehemu, katika chumba cha bweni lao wanaishi wanafunzi wanne ambapo siku ya tarehe 6/03/2016 hakukuwa na umeme na uliporudi umeme wanafunzi hao walianza kugombani chaja hiyo ya simu ugomvi uliopelekea kuanza kupigana na  ndipo BASILI MSABILA kujeruhiwa kwa chuma chenye ncha kali kichwani na kupelekwa Hospitali ya Mkoa wa Dodoma kwa matibabu na kufariki dunia akiwa kwenye matibabu siku iliyofuata. Mtuhumiwa amekamatwa na uchunguzi zaidi kuhusu tukio hilo unendelea.

Vilevile Kamanda MAMBOSASA amesema tukio lingine limetokea tarehe 07.03.2016 majira ya saa 21:00hrs huko eneo la Kisasa Manispaa ya Dodoma ambapo mtu mmoja mwanaume asiyefahamika jina mwenye umri kati ya miaka 23-25 aliuwawa kwa kukatwa na kitu chenye ncha kali shingoni na mtu/watu waliojichukulia sheria mkononi kwa tuhuma za kujaribu kuvunja dirisha la nyumba akiwa na wenzake waliofanikiwa kukimbia. Uchunguzi unaendelea na Juhudi za kuwatafuta watu waliohusika na mauaji hayo zinafanyika.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma LAZARO MAMBOSASA – ACP ametoawito kwa wananchi wa Dodoma kutojichukulia sheria mkononi na kutofanya mauaji ya kikatili dhidi ya watu kwa tuhuma nyepesi kwa kisingizio cha watu wenye hasira kali. Vitendo hivi havitavumilika na sheria zifuatwe kila mtu ana haki ya kuishi na kujitetea mbele ya sheria.

    RPC Dodoma LAZARO MAMBOSASA - ACP akionyesha mitambo ya kutengenezea bunduki         hizo.

    RPC Dodoma LAZARO MAMBOSASA - ACP akionyesha mtambo wa kutengeneza bunduki           haramu.

    RPC Dodoma LAZARO MAMBOSASA - ACP akionyesha silaha aina ya gobore zilizokamatwa       katika msako huo.

    Kamanda wa Polisi Dodoma LAZARO MAMBOSASA akionyesha goroli zitumikazo katika               magobore hayo.

    RPC Dodoma Kamishna Msaidizi wa Polisi LAZARO MAMBOSASA - ACP