Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dk. John Magufuli amesikitishwa na mauaji ya kinyama yaliyotokea hivi karibuni baada ya watu
saba wa familia moja waliokatwa mapanga katika Kijiji cha Sima wilayani
Sengerema mkoani Mwanza.
kutokana na tukio hilo kutokea Rais Magufuli ameviagiza vyombo vya dola kuwasaka kwa
nguvu zote, watu waliohusika na mauaji hayo na kuhakikisha wanatiwa
mbaroni hara iwezekanavyo.
Akitoa
salamu za pole nyumbani kwa wafiwa Makamu wa Rais, Samia Suluhu
Hassan, amesema Rais Magufuli ameguswa na tukio hilo
makamu wa raisi amesema
Rais Magufuli ametaka wahusika wote wakamatwe ndani ya kipindi kifupi,
kwa sababu mauaji ya aina hiyo hayakubaliki hata kidogo na hawezi kuvumilia katika nchi yake.
No comments:
Post a Comment