Pages

Friday, 13 May 2016

WAZIRI WA HABARI, UTAMADUNI, SANAA NA MICHEZO Mh. NAPE NNAUYE ASOMA BAJETI YA WIZARA YAKE BUNGENI DODOMA

   Waziri wa Habari, Utamaduni, sanaa na Michezi Mh. Nape Nnauye amewasilisha bungeni makadilio ya mapato na matumizi ya fedha kwa mwaka 2061/2017 kwa wizara hiyo na kusema sekta ya maendeleo ya sanaa imefanikiwa kwa mwaka 2016 kwa kufanikiwa kwa wasanii wawili nchini kushinda tuzo za African Magic Viewers Choice Awards - AMVCA 2016 HUKO Nigeria.

   Wasanii hao ni Bw. Single Mtambalike (Richie) Filamu ya Kitendawili kipengele cha filamu bora ya lugha ya asili(Kiswahili) na Bi. Elizabeth Michael (Lulu) Filamu ya Mapenzi ya mungu kipengele cha Filamu bora Afrika Mashariki.

   Vilevile Mh. Nape amesema muongozaji wa filamu ya "Dogo Masai" Bw. Timoth Cornad alipata tuzo ya Calfonia Viewers Choice Awards huko marekani. Kwa upande wa muziki wasanii wanne walipata tuzo mbalimbali nje ya nchi.

   Jumla ya tuzo 20 zimepatikana kutoka kwa wasanii wafuatao; Bw. Nassib Abdul (Diamond) tuzo 17, Bi. Vanessa Mdee tuzo 1, Bw. Malima Mayunga tuzo 1 na Bw. Omary Nyembe (Ommy Dimpoz) tuzo 1.

   Aidha Mh. Nape amesema Wizara kwa kushirikiana na wadau wa sanaa ilifanikisha wasanii nchini kupata tuzo za sanaa kwa mwaka 2015/2016. Tuzo zilizotolewa ni "Tanzania Kilimanjaro Music Awards" - 34, Tuzo za siku ya Msanii - 4 na Tuzo za watu 13.

  Waziri wa Habari, Utamaduni, sanaa na Michezi Mh. Nape Nnauye akiwasilisha   Bungeni Makadilio ya mapato na matumizi ya Fedha kwa mwaka 2016/2017.



    Mbunge wa Mbeya Mjini Mh. Joseph Mbilinyi - SUGU akitoa hotuba ya kambi rasmi ya    upinzani kuhusu makadilio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ambaye pia ni waziri kivuli wa wizara hiyo.

   Akitoa hotuba kwa kambi rasmi ya upinzani Mh. Joseph Mbilinyi amewashukuru wananchi wa mbeya mjini kwa kumchagua na kufanikiwa kuwa msanii wa kwanza wa Hip Hop duniani kuwa Mbunge na kumtaja aliyefuata kuwa ni Mh. Joseph Haule - Prof. Jay.

 

 Msanii wa Filamu nchini Wema sepetu akifuatilia kwa makini hotuba ya Mh. Nape bungeni Dodoma.

 

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mh. Nape Nnauye akiwa katika picha ya paomja na wasanii mbalimbali waliokuwepo bungeni wakati akiwasilisha makadilio ya mapato na matumizi ya wizara yake.


Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mh. Nape Nnauye akiwa katika picha ya pomoja na mabloger mbalimbali mbele ya lango kuu la bunge.


Msanii wa Filamu JB akiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi wa shule ya sekondari ya Magubike iliyopo Mkoani Morogoro waliokuja bungeni kujifunza namna ya bunge linavyoendeshwa.


Msanii Richi Richi na JB wakiwa katika picha na wadau wa Filamu bungeni Mjini Dodoma walikuja kusikiliza hotuba ya Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo iliyowasilishwa leo Bungeni.

 

No comments:

Post a Comment