Pages

Friday, 13 May 2016

HRW NA AMNESTY ZAITAKA UGANDA KUMKAMATA AL-BASHIR

 
  
 Mashirika ya kimataifa ya kutetea haki za binadamu yameitaka serikali ya Uganda kumkamata Rais Omar al-Bashir wa Sudan na kumkabidhi kwa Mahakama ya Kimataifa ya Jinai ICC, kwa tuhuma za mauaji ya kimbari katika eneo la Darfur na jinai dhidi ya binadamu. 
Mashirika ya kutetea haki za binadamu ya Amnesty International na Human Rights Watch yameitaka serikali ya Uganda kutekeleza wajibu wake wa kimataifa na kumkabidhi kwa mahakama ya ICC, Rais wa Sudan ambaye alienda mjini Kampala kuhudhuria hafla ya kuapishwa Rais Yoweri Museveni. 

Muthoni Wanyeki, Mkurugenzi wa Amnesty International katika kanda ya Afrika Mashariki, Pembe ya Afrika na eneo la Maziwa Makuu amesema Uganda ni mwanachama wa Mkataba wa Roma uliobuni Mahakama ya Kimataifa ya Jinai ICC na hivyo, iwapo itafeli kumkabidhi Rais wa Sudan, itakuwa imeshindwa kutekeleza wajibu wake wa kimataifa. Hii ni katika hali ambayo, baada ya kula kiapo hapo jana, Rais Museveni aliikashifu ICC na kusema kuwa mahakama hiyo imegeuka na kuwa chombo cha kuwadhalilisha viongozi wa Kiafrika huku ikiwasaza viongozi makatili wa nchi za Magharibi

. Kauli ya Museveni iliwaghadhabisha wajumbe wa Marekani na Umoja wa Ulaya waliokuwa wamehudhuria sherehe za kuapishwa kwake katika Viwanja vya Kololo jijini Kampala na kuwafanya kuondoka kwenye hafla hiyo. 

Itakumbukwa kuwa, serikali ya Afrika Kusini ilikataa kumkamata Rais Omar al-Bashir ambaye alishiriki mkutano wa viongozi wa Afrika uliofanyika mjini Johannesburg Julai mwaka jana. 

Aidha Kenya ilipuuza wito wa kumkamata na kumkabidhi kiongozi huyo kwa Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai ICC anakotakiwa kujibu tuhuma za mauaji ya kimbari katika eneo la Darfur na jinai dhidi ya binadamu; alipohudhuria sherehe za kuapishwa Rais Uhuru Kenyatta wa nchi hiyo ya Afrika Mashariki mwaka 2013.

RAISI MAGUFULI ATAKA WATU WALIOUWA WATU SABA WA FAMILIA MOJA WAKAMATWE MARA MOJA

  
Rais   wa jamhuri ya muungano wa Tanzania  Dk. John Magufuli amesikitishwa na mauaji ya kinyama yaliyotokea hivi karibuni baada ya  watu saba wa familia moja waliokatwa mapanga katika Kijiji cha Sima wilayani Sengerema mkoani Mwanza.

kutokana na tukio hilo kutokea  Rais Magufuli ameviagiza vyombo vya dola kuwasaka kwa nguvu zote, watu waliohusika na mauaji hayo na kuhakikisha wanatiwa mbaroni hara iwezekanavyo.

Akitoa salamu za pole nyumbani kwa wafiwa  Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan, amesema Rais Magufuli ameguswa na tukio hilo 



makamu wa raisi amesema Rais Magufuli ametaka wahusika wote wakamatwe ndani ya kipindi kifupi, kwa sababu mauaji ya aina hiyo hayakubaliki hata kidogo na hawezi kuvumilia katika nchi yake.

WAZIRI WA HABARI, UTAMADUNI, SANAA NA MICHEZO Mh. NAPE NNAUYE ASOMA BAJETI YA WIZARA YAKE BUNGENI DODOMA

   Waziri wa Habari, Utamaduni, sanaa na Michezi Mh. Nape Nnauye amewasilisha bungeni makadilio ya mapato na matumizi ya fedha kwa mwaka 2061/2017 kwa wizara hiyo na kusema sekta ya maendeleo ya sanaa imefanikiwa kwa mwaka 2016 kwa kufanikiwa kwa wasanii wawili nchini kushinda tuzo za African Magic Viewers Choice Awards - AMVCA 2016 HUKO Nigeria.

   Wasanii hao ni Bw. Single Mtambalike (Richie) Filamu ya Kitendawili kipengele cha filamu bora ya lugha ya asili(Kiswahili) na Bi. Elizabeth Michael (Lulu) Filamu ya Mapenzi ya mungu kipengele cha Filamu bora Afrika Mashariki.

   Vilevile Mh. Nape amesema muongozaji wa filamu ya "Dogo Masai" Bw. Timoth Cornad alipata tuzo ya Calfonia Viewers Choice Awards huko marekani. Kwa upande wa muziki wasanii wanne walipata tuzo mbalimbali nje ya nchi.

   Jumla ya tuzo 20 zimepatikana kutoka kwa wasanii wafuatao; Bw. Nassib Abdul (Diamond) tuzo 17, Bi. Vanessa Mdee tuzo 1, Bw. Malima Mayunga tuzo 1 na Bw. Omary Nyembe (Ommy Dimpoz) tuzo 1.

   Aidha Mh. Nape amesema Wizara kwa kushirikiana na wadau wa sanaa ilifanikisha wasanii nchini kupata tuzo za sanaa kwa mwaka 2015/2016. Tuzo zilizotolewa ni "Tanzania Kilimanjaro Music Awards" - 34, Tuzo za siku ya Msanii - 4 na Tuzo za watu 13.

  Waziri wa Habari, Utamaduni, sanaa na Michezi Mh. Nape Nnauye akiwasilisha   Bungeni Makadilio ya mapato na matumizi ya Fedha kwa mwaka 2016/2017.



    Mbunge wa Mbeya Mjini Mh. Joseph Mbilinyi - SUGU akitoa hotuba ya kambi rasmi ya    upinzani kuhusu makadilio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ambaye pia ni waziri kivuli wa wizara hiyo.

   Akitoa hotuba kwa kambi rasmi ya upinzani Mh. Joseph Mbilinyi amewashukuru wananchi wa mbeya mjini kwa kumchagua na kufanikiwa kuwa msanii wa kwanza wa Hip Hop duniani kuwa Mbunge na kumtaja aliyefuata kuwa ni Mh. Joseph Haule - Prof. Jay.

 

 Msanii wa Filamu nchini Wema sepetu akifuatilia kwa makini hotuba ya Mh. Nape bungeni Dodoma.

 

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mh. Nape Nnauye akiwa katika picha ya paomja na wasanii mbalimbali waliokuwepo bungeni wakati akiwasilisha makadilio ya mapato na matumizi ya wizara yake.


Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mh. Nape Nnauye akiwa katika picha ya pomoja na mabloger mbalimbali mbele ya lango kuu la bunge.


Msanii wa Filamu JB akiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi wa shule ya sekondari ya Magubike iliyopo Mkoani Morogoro waliokuja bungeni kujifunza namna ya bunge linavyoendeshwa.


Msanii Richi Richi na JB wakiwa katika picha na wadau wa Filamu bungeni Mjini Dodoma walikuja kusikiliza hotuba ya Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo iliyowasilishwa leo Bungeni.

 

Thursday, 12 May 2016

DIAMOND NA MAFIKIZOLO NDANI YA MJENGO WA BUNGE

    Bunge la Tanzania Mkutano wa 3 kikao cha 18

    Diamond na Mafikizolo wakiwa VIP Bungeni baada ya kualikwa na Waziri wa Habari,    
    Sanaa na  Michezo Mh. Nape Nauye.
    Diamond, Mafikizolo na Waziri wa Habari, Sanaa na Michezo Mh. Nape Nauye pamoja na   
    Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira Mh. January Makamba
    kwenye picha ya pamoja mbele ya lango kuu la bunge.

   Diamond akiwa na wapenzi mbalimbali wa burudani pamoja na wabunge katika picha ya  
    pamoja mbele ya lango kuu la bunge.


INTERVIEW YA MAFIKIZOLO NA WAANDISHI WA HABARI BUNGENI MJINI DODOMA KBLA YA KUFANYA SHOW UDOM.





PIA NAE DIAMOND ALISEMA HAYA ANGALIA INTERVIEW YAKE HAPA CHINI