Thursday, 1 September 2016
KUPATWA KWA JUA TANZANIA
Tukio la kupatwa kwa jua limetokea leo katika Kijiji cha Rujewa Wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya, Katibu wa Mila wa katika kijiji hicho Mwanasimtwa Mwagongo amesema tukio hilo ni ishara ya Mwenyezi Mungu kuukubali uongozi wa Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais John Magufuli.
Hii itakuwa ni mara ya kwanza Tanzania kutokea tukio hilo tangu Aprili 18, 1977 na tukio kama hilo la kihistoria linatarajiwa kutokea tena nchini Mei 21, 2031.
Mbali ya Rujewa ambako watu wameona tukio hili la kupatwa kwa jua kwa asilimia 97 sawa na miji ya Makambako, Masasi, Mbeya, Tunduru, Njombe na Sumbawanga, miji mingine ambayo imeona tukio hilo kwa ukaribu zaidi wa asilimia 96 ni Katavi, Nachingwea na Songea ikifuatiwa na Kigoma, Iringa, Mtwara na Lindi.
Akizungumza na waandishi habari za Utalii na Uwekezaji Tanzania (TAJATI) nyumbani kwake katika Kata ya Isisi, Mwagongo amesema tukio hilo la kupatwa kwa jua nchini si mkosi, bali ni sawa na taa iliyokuwa imezimika na sasa imewashwa na kuongeza kuwa, ni ishara kuwa Mungu ameukubali utawala uliopo madarakani na ndiyo sababu ametoa giza na kuleta nuru.
Amewaasa viongozi wa dini zote kote nchini kuliombea tukio hilo ili lifanyike na kupita kwa amani na pasiwepo na uvunjifu wa amani utakaosababisha jamii kutoa tafsiri ya tofauti baada ya tukio hili la kihistoria ambalo limefanyika kati ya saa 4.15 asubuhi hadi saa 8.00 mchana.
baada ya tukio hilo, wazee wa kimila watachinja ng’ombe kwa ajili ya kumshukuru Mungu kwa neema ya tukio hilo na pia kumwomba aiepushe jamii na madhara yoyote yanayoweza kujitokeza.
Hapo zamani watoto walikuwa hawaruhusiwi kutoka nje siku ya tukio hili. Wazee waliamini ni ajali ya kugongana jua na mwezi na wanaoumia ni wanadamu hasa watoto kwa kusababishiwa milipuko ya magonjwa mbalimbali
Lakini kwa sasa tunatambua kuwa ni tukio la kisayansi na kutokea kwenye eneo letu ni neema kutoka kwa Mungu. Kupitia tukio hili dunia itaijua Tanzania, itaijua Mbarali na itaijua Rujewa. Ni tukio ambalo limetutangaza.
Monday, 29 August 2016
MKUTANO WA 36 WA NCHI ZA SADC KUFANYIKA LEO HUKO SWAZILAND
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe SAMIA SULUHU HASSAN amewasili mjini Mbabane -
Swaziland leo kwa ajili ya kuhudhuria mkutano wa 36 wa Wakuu wa nchi na
serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika- SADC.
Makamu wa Rais SAMIA SULUHU HASSAN atamwakilisha Rais wa Jamhuri ya
Muungano Tanzania Dakta JOHN MAGUFULI katika mkutano huo ambao unatarajia kufanyika leo tarehe 29 Agosti 2016 ambapo Tanzania inatarajiwa
kukabidhiwa nafasi ya Uenyekiti wa Jumuiya hiyo.
Mkutano huo wa 36 wa SADC ni maalum kwa wakuu wa nchi na serikali
wanaounda Kamati ya siasa, Ulinzi na usalama ambao watajadili kwa kina
hali ya siasa na usalama, demokrasia na maombi ya Burundi na Comoro kwa
ajili ya kujiunga na SADC.
Makamu wa Rais Mhe, SAMIA SULUHU HASSAN katika msafara wake ameongozana na Waziri wa Mambo ya nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa Augustine Mahiga, Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji John Mwijage na Waziri wa Biashara, Viwanda na Masoko wa serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Amina Salum Ali.
Makamu wa Rais Mhe, SAMIA SULUHU HASSAN katika msafara wake ameongozana na Waziri wa Mambo ya nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa Augustine Mahiga, Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji John Mwijage na Waziri wa Biashara, Viwanda na Masoko wa serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Amina Salum Ali.
Tuesday, 26 July 2016
SIKUKUU YA MASHUJAA YAFANYIKA KITAIFA MKONI DODOMA
TAZAMA PICHA ZA SIKUKUU YA MASHUJAA ILIYOFANYIKA KITAIFA MKONI DODOMA NA KUHUDHURIWA NA VIONGOZI MBALIMBALI.
Friday, 13 May 2016
HRW NA AMNESTY ZAITAKA UGANDA KUMKAMATA AL-BASHIR
Mashirika ya kimataifa ya kutetea haki za
binadamu yameitaka serikali ya Uganda kumkamata Rais Omar al-Bashir wa
Sudan na kumkabidhi kwa Mahakama ya Kimataifa ya Jinai ICC, kwa tuhuma
za mauaji ya kimbari katika eneo la Darfur na jinai dhidi ya binadamu.
Mashirika ya kutetea haki za binadamu ya Amnesty International
na Human Rights Watch yameitaka serikali ya Uganda kutekeleza wajibu
wake wa kimataifa na kumkabidhi kwa mahakama ya ICC, Rais wa Sudan
ambaye alienda mjini Kampala kuhudhuria hafla ya kuapishwa Rais Yoweri
Museveni.
Muthoni Wanyeki, Mkurugenzi wa Amnesty International katika kanda ya
Afrika Mashariki, Pembe ya Afrika na eneo la Maziwa Makuu amesema Uganda
ni mwanachama wa Mkataba wa Roma uliobuni Mahakama ya Kimataifa ya
Jinai ICC na hivyo, iwapo itafeli kumkabidhi Rais wa Sudan, itakuwa
imeshindwa kutekeleza wajibu wake wa kimataifa. Hii ni katika hali
ambayo, baada ya kula kiapo hapo jana, Rais Museveni aliikashifu ICC na
kusema kuwa mahakama hiyo imegeuka na kuwa chombo cha kuwadhalilisha
viongozi wa Kiafrika huku ikiwasaza viongozi makatili wa nchi za
Magharibi
. Kauli ya Museveni iliwaghadhabisha wajumbe wa Marekani na
Umoja wa Ulaya waliokuwa wamehudhuria sherehe za kuapishwa kwake katika
Viwanja vya Kololo jijini Kampala na kuwafanya kuondoka kwenye hafla
hiyo.
Itakumbukwa kuwa, serikali ya Afrika Kusini ilikataa kumkamata Rais
Omar al-Bashir ambaye alishiriki mkutano wa viongozi wa Afrika
uliofanyika mjini Johannesburg Julai mwaka jana.
Aidha Kenya ilipuuza
wito wa kumkamata na kumkabidhi kiongozi huyo kwa Mahakama ya Kimataifa
ya Makosa ya Jinai ICC anakotakiwa kujibu tuhuma za mauaji ya kimbari
katika eneo la Darfur na jinai dhidi ya binadamu; alipohudhuria sherehe
za kuapishwa Rais Uhuru Kenyatta wa nchi hiyo ya Afrika Mashariki mwaka
2013.
RAISI MAGUFULI ATAKA WATU WALIOUWA WATU SABA WA FAMILIA MOJA WAKAMATWE MARA MOJA
Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dk. John Magufuli amesikitishwa na mauaji ya kinyama yaliyotokea hivi karibuni baada ya watu
saba wa familia moja waliokatwa mapanga katika Kijiji cha Sima wilayani
Sengerema mkoani Mwanza.
kutokana na tukio hilo kutokea Rais Magufuli ameviagiza vyombo vya dola kuwasaka kwa
nguvu zote, watu waliohusika na mauaji hayo na kuhakikisha wanatiwa
mbaroni hara iwezekanavyo.
Akitoa
salamu za pole nyumbani kwa wafiwa Makamu wa Rais, Samia Suluhu
Hassan, amesema Rais Magufuli ameguswa na tukio hilo
makamu wa raisi amesema
Rais Magufuli ametaka wahusika wote wakamatwe ndani ya kipindi kifupi,
kwa sababu mauaji ya aina hiyo hayakubaliki hata kidogo na hawezi kuvumilia katika nchi yake.
WAZIRI WA HABARI, UTAMADUNI, SANAA NA MICHEZO Mh. NAPE NNAUYE ASOMA BAJETI YA WIZARA YAKE BUNGENI DODOMA
Waziri wa Habari, Utamaduni, sanaa na Michezi Mh. Nape Nnauye amewasilisha bungeni makadilio ya mapato na matumizi ya fedha kwa mwaka 2061/2017 kwa wizara hiyo na kusema sekta ya maendeleo ya sanaa imefanikiwa kwa mwaka 2016 kwa kufanikiwa kwa wasanii wawili nchini kushinda tuzo za African Magic Viewers Choice Awards - AMVCA 2016 HUKO Nigeria.
Wasanii hao ni Bw. Single Mtambalike (Richie) Filamu ya Kitendawili kipengele cha filamu bora ya lugha ya asili(Kiswahili) na Bi. Elizabeth Michael (Lulu) Filamu ya Mapenzi ya mungu kipengele cha Filamu bora Afrika Mashariki.
Vilevile Mh. Nape amesema muongozaji wa filamu ya "Dogo Masai" Bw. Timoth Cornad alipata tuzo ya Calfonia Viewers Choice Awards huko marekani. Kwa upande wa muziki wasanii wanne walipata tuzo mbalimbali nje ya nchi.
Jumla ya tuzo 20 zimepatikana kutoka kwa wasanii wafuatao; Bw. Nassib Abdul (Diamond) tuzo 17, Bi. Vanessa Mdee tuzo 1, Bw. Malima Mayunga tuzo 1 na Bw. Omary Nyembe (Ommy Dimpoz) tuzo 1.
Aidha Mh. Nape amesema Wizara kwa kushirikiana na wadau wa sanaa ilifanikisha wasanii nchini kupata tuzo za sanaa kwa mwaka 2015/2016. Tuzo zilizotolewa ni "Tanzania Kilimanjaro Music Awards" - 34, Tuzo za siku ya Msanii - 4 na Tuzo za watu 13.
Waziri wa Habari, Utamaduni, sanaa na Michezi Mh. Nape Nnauye akiwasilisha Bungeni Makadilio ya mapato na matumizi ya Fedha kwa mwaka 2016/2017.
Mbunge wa Mbeya Mjini Mh. Joseph Mbilinyi - SUGU akitoa hotuba ya kambi rasmi ya upinzani kuhusu makadilio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ambaye pia ni waziri kivuli wa wizara hiyo.
Akitoa hotuba kwa kambi rasmi ya upinzani Mh. Joseph Mbilinyi amewashukuru wananchi wa mbeya mjini kwa kumchagua na kufanikiwa kuwa msanii wa kwanza wa Hip Hop duniani kuwa Mbunge na kumtaja aliyefuata kuwa ni Mh. Joseph Haule - Prof. Jay.
Msanii wa Filamu nchini Wema sepetu akifuatilia kwa makini hotuba ya Mh. Nape bungeni Dodoma.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mh. Nape Nnauye akiwa katika picha ya pomoja na mabloger mbalimbali mbele ya lango kuu la bunge. |
Msanii wa Filamu JB akiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi wa shule ya sekondari ya Magubike iliyopo Mkoani Morogoro waliokuja bungeni kujifunza namna ya bunge linavyoendeshwa. |
Msanii Richi Richi na JB wakiwa katika picha na wadau wa Filamu bungeni Mjini Dodoma walikuja kusikiliza hotuba ya Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo iliyowasilishwa leo Bungeni. |
Thursday, 12 May 2016
DIAMOND NA MAFIKIZOLO NDANI YA MJENGO WA BUNGE
Sanaa na Michezo Mh. Nape Nauye.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira Mh. January Makamba
kwenye picha ya pamoja mbele ya lango kuu la bunge.
pamoja mbele ya lango kuu la bunge.
INTERVIEW YA MAFIKIZOLO NA WAANDISHI WA HABARI BUNGENI MJINI DODOMA KBLA YA KUFANYA SHOW UDOM.
PIA NAE DIAMOND ALISEMA HAYA ANGALIA INTERVIEW YAKE HAPA CHINI
Subscribe to:
Posts (Atom)