Pages

Sunday, 28 July 2013

MWANAMUZIKI WA DANCE PAPY MARAY AMBAE AMEWAHI KUTUMIKIA BAND MBALIMBALI AMEAMUA KUJA KIVINGINE

Papy Maray ambae amewahi kutamba na band mbalimbali hapa nchini Tanzania kama vile Diamond musicaStono mayeyasika,na Akudo Impact ameamua kutoka kivyake na tungo mbali mbali akiwa kama solo artist
papy maray ambae aliondoka na kutimukia ughaibuni ambapo alikuwa dubai kisha kurejea nchini kwao DRC na kukaa huko kwa muda mara baada ya kutoka Akudo impact, kwa sasa yupo nchini akiwa bado hajajua ni band gani ataitumiakia hivyo ameamu kutunga nyimbo zake akiwa kama solo artist ambazo zitakuwa zikikamilisha album yake ambayo anatarajia kuitoa, hivyo mpaka sasa bado anakamilisha baadhi ya nyimbo ili kumalizia  album yake

mpaka sasa Maray ameshakamilisha nyimbo nne ambazo ni Passport-pirate akiwa anamaanisha pasport feki,Deseption akiwa anamaanisha huzuni ,Mwasi mabe akimaanisha mwanamuke mwenyetabia mbaya pamoja na Maskini hizo ndio nyimbo ambazo ameziimba akiwa kama solo artist

Maray amesema mpaka sasa anampango wa kurudi kati ya band mbili ambazo ni akudo,au diamond lakini mpaka sasa bado hajajua ataelekea wapi na kuseama mtu atakae hitaji shoo zake yupo huru kwani bado hajamilikiwa na band yeyote

No comments:

Post a Comment