Pages

Sunday, 28 July 2013

MWANAMUZIKI WA DANCE PAPY MARAY AMBAE AMEWAHI KUTUMIKIA BAND MBALIMBALI AMEAMUA KUJA KIVINGINE

Papy Maray ambae amewahi kutamba na band mbalimbali hapa nchini Tanzania kama vile Diamond musicaStono mayeyasika,na Akudo Impact ameamua kutoka kivyake na tungo mbali mbali akiwa kama solo artist
papy maray ambae aliondoka na kutimukia ughaibuni ambapo alikuwa dubai kisha kurejea nchini kwao DRC na kukaa huko kwa muda mara baada ya kutoka Akudo impact, kwa sasa yupo nchini akiwa bado hajajua ni band gani ataitumiakia hivyo ameamu kutunga nyimbo zake akiwa kama solo artist ambazo zitakuwa zikikamilisha album yake ambayo anatarajia kuitoa, hivyo mpaka sasa bado anakamilisha baadhi ya nyimbo ili kumalizia  album yake

mpaka sasa Maray ameshakamilisha nyimbo nne ambazo ni Passport-pirate akiwa anamaanisha pasport feki,Deseption akiwa anamaanisha huzuni ,Mwasi mabe akimaanisha mwanamuke mwenyetabia mbaya pamoja na Maskini hizo ndio nyimbo ambazo ameziimba akiwa kama solo artist

Maray amesema mpaka sasa anampango wa kurudi kati ya band mbili ambazo ni akudo,au diamond lakini mpaka sasa bado hajajua ataelekea wapi na kuseama mtu atakae hitaji shoo zake yupo huru kwani bado hajamilikiwa na band yeyote

Thursday, 18 July 2013

NGULI WA MUZIKI WA DANCE DUNIANI MBUTA LIKASU MBIONI KUACHIA ALBUM MPAYA

Mbuta Likasu ambae amewahi kutamba na nyimbo mbalimbali duniani  zikiwa ni pamoja na position ,cris totale ,fete des chiens,attention obus Grace a Deau,Jose pila na nyingine nyingi  kutokana na umahili wake katika muziki wa dance amesema kwa sasa yuko tayari kuachia album mpya

Mbuta Likasu ambae ni mtu mwenye vituko mbali mbali amesema ifikapo augost au september mwaka huu ataachia album yake ambayo inajulikana kwa jina la carnival ambapo kuna vol.1 na vol.2 ambazo ni mpya kabisa

Mbali na carnival Likasu amsema ana album nyingine za mwanzo ambazo ni attention obus ikiwa ni album yake ya kwanza souve qui peut ambayo ni album yake ya pili na sasa anaachia carnival ikiwa ni album yake ya tatu ambayo anatarajia kuiachia hivi karibuni

Muta Likasu ambae kwa sasa yuko mjini  Kinshasa anaendelea na shoo zake mbali mbali mjini humo pamoja na  Congo brazzaville

Wednesday, 17 July 2013

MWANAMUZI WA MUSIC WA DANCE WILLY FOLOLO AWAZIA KUWA NA BAND YAKE

Mwanamuziki nyimbo za dance nchini Tanzania Willy Fololo amesema kwa sasa anamatarajio makubwa ya kuanzisha band yake mwenyewe.

Fololo amesema kutokana na kufanya kazi ya musiki kwa muda mrefu na band mbalimbali nchini hapa  na kutokana na uzoefu aliokuwa nao anauwezo wa kumili band yake.

Fololo amesema hayo alipokuwa akizungumza na safu ya Queen Jozzee na africa moto, amesema kwa sasa ana album yake inayojulikana kama Fololowise ambayo mpaka sasa inanyimbo kumi na mbili  akiwa ameimba kwa mtimdo mbalimbali ikiwa ni pamoja na mtindo wa Zoukou ,Rhumba ,Sebene na Dancehall, amesema ni moto wa kuotea mbali

mbali na hayo Fololo ameakmilisha video yake kali ya afrobeats ambayo ni tishio kubwa amesema ngoma hiyo inaitwa leo akiwa amemshirisha ghetto grade warrios kutoka mashariki

hata hivyo Fololo amesema kutokana na album yake kuwa mpya kwa sasa anajiandaa kuisambaza katika media mbalimbali na kuifanyia promo ya kutosha kabla haijafika sokoni