Pages

Wednesday, 19 August 2015

MAMIA YA WATU WAMEJITOKEZA KUUAGA MWILI ALPHONCE MISIME AMBAYE NI BABA WA RPC DODOMA MKOANI HUMO.

Mamia ya watu wamejitokeza kumuaga Baba mzani wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma DAVID MISIME - SACP aliyefariki jumamosi jioni na kuagwa jumanne nyumbani kwa RPC Uzunguni Dodoma kisha baadaye kusafirishwa kuelekea Moshi kwa mazishi.

Kamanda MISIME amewashukuru sana watuwaliojitokeza kuuaga mwili wa babayake na kuwasisitizia kusali na kujiandaa kiroho kwani safari ni moja.

Bwana ametoa na bwana ametwaa jina lake lihimidiwe.


      RPC Dodoma DAVID MISIME akitoa heshima za mwisho wa Baba yake ALPHONCE MISIME.

                 Familia ya RPC Dodoma DAVID MISIME wakiwa katika ibada hiyo


       Familia ya RPC Dodoma wakitoa heshima za mwisho tayari kwa kusafirishwa kuelekea Moshi kwa
       mazishi.

 
     Paroko wa Kanisa kuu la Mt. PAULO WA MSALABA akinyunyizia maji ya baraka kama heshima ya
     mwisho ya kuuaga mwili wa marehemu.

         Ibada ya kuuaga mwili wa marehemu ALPHONCE MISIME ambaye ni Baba wa RPC Dodoma   
         iliyofanyika nyumbani kwake uzungunu Dodoma.

     Mkuu wa Mkoa Dodoma CHIKU GALAWA akitoa shukrani kwa niaba ya kamati ya ulinzi na usalama
     ya Mkoa.
                    RPC Dodoma DAVID MISIME - SACP akitoa shukrani za dhati katika ibada hiyo.


     Afisa mnadhimu (S.O 1) Dodoma D. MNYAMBUGA - ACP akitoa neno la shukrani katika ibada hiyo 
     ya kuuaga mwili wa ALPHONCE MISIME ambaye ni Baba wa RPC Dodoma.

      Padri CHESCO akitoa neno la shurani kwa niaba ya Askofu mkuu wa jimbo la Dodoma katika ibada
      hiyo.

      OCD Dodoma THADEUS MALINGUMU - SP wa pili katika picha akitoa heshma za mwisho kwa 
      mwili wa marehemu.
     Mwili wa marehemu ukiwa umebebwa kuelekea kwenye gari tayari kwa kusafirishwa kwenda Moshi
     kwaajili ya mazishi.

Monday, 17 August 2015

CHAZ BABA ASIMAMISHWA KAZI TAKRIBANI WIKI 3 KATIKA BAND YA MASHUJAA



Meneja wa Band ya Mashujaa Musica Sospete martin amekiri kusimamishwa kazi kwa muda wa wiki tatu kwa raisi wa band hiyo ya mashujaa Charz baba.
               Manager wa Mashujaa Musica Martin Sospete

sospeter kisa cha kusimamishwa kwa rais huyo wa band ya mashujaa nikutokana na utovu wa nidhamu kwani ALIKUWA HAENDI KAZINI LAKINI BADALA YA HAPO ANAONEKANA KWENYE MAOvNYESHO YA BAND NYINGINE AMESEMA Sospete meneja wa mashujaa

Sospeter amesema walikuwa wakimuona kwenye mitandao ya kijamii lakini huku hashiriki katika band yake hivyo kama uongozi wa band hiyo waliamua kukaa na kujadili ni aina gani ya adhabu ndipo waliamua kumpa adhabu hiyo 

Sospeter amesema kuwa Chaz kama kiongozi hakustahili kufanya hivyo anaamani adhabu waliompa inaweza kuwafanya watanzania kuamini kuwa hata kiongozi anatakiwa kupewa adhabu.

 baada ya kusimamishwa kwa muda wa mwezi mzima Rais wa 
Mashujaa Band Chaz Baba amesema amekubali adhabu ya kusimamishwa kazi na bendi hiyo lakini akatahadharisha kuwa ni lazima atapanda majukwaa ya bendi nyingine ili kujikimu
                        raisi wa band ya mashujaa musica Chaz Baba

akizungumza na safu yetu ya afrika moto Chaz Baba amesema katika kipindi hiki alichosimamishwa kazi ni lazima atashiriki maonyesho ya bendi nyingine ili kujipatia rizki sambamba na kulinda kipaji chake lakini Chaz baba amekiri kusimamishwa kwa muda wa wiki tatu kwa kosa la kupanda jukwaa la Twanga Pepeta wamenisimamisha kazi, lakini badaa ya hapo nitarejea kazini, lakini katika kipindi hiki cha adhabu sitakubali kubaki nyumbani, nitakwenda kushiriki maonyesho ya bendi zingine kwani muziki ndio kazi yangu, unaponisimamisha kwa wiki tatu, unakuwa hinitakii mema,

lakini katika mazungumzo yangu na charz baba nilijarinu kuuliza swali la yeye baada ya kumaliza adhabu yake yuko tayari kurudi katika band yake kwa ajili ya kuitumia alijibu kuwa ataangalia kama itawezekana

Saturday, 15 August 2015

MGANGA FEKI AKAMATWA MOANI DODOMA AKIWA NA VIFAA TIBA PAMOJA NA DAWA






 MGANGA FEKI AKMATWA WILAYANI KONGWA MKOA WA DODOMA  AKITOA HUDUMA KWA WAGONJWA.


    Mganga feki alikiekamatwa na Jeshi la Polisi Bw: Abdalla

                               

        Nyumba anayotumia Bw: Abdalla kwa kutibu Wagonjwa


                Vifaa tiba na dawa alizokutwa nazo Daktari huyo feki

mnamo Tarehe 12.08.2015 majira ya 15:00 mchana katika kijiji cha Nyerere Kata ya Hogoro, Tarafa ya Zoissa Wilaya ya Kongwa, mtu aliyefahamika kwa jina na MOHAMED ABDALLAH, Miaka 35, Mkazi wa Katesh Wilaya ya Kiteto Mkoa wa Manyara alikutwa akitoa huduma ya matibabu kwa wagonjwa zaidi ya 20 akiwa hana kibali wala leseni ya kutoa huduma hiyo.

akithibitisha kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo kamishina msaidizi mwandami wa polisi mkoani Dodoma SACP-David Misime Baada ya taarifa za siri kulifikia Jeshi la Polisi, mtuhumiwa alikamatwa katika nyumba ambayo haistahili kufanyiwa shughuli za matibabu ambayo ni mali ya SIKITU MAGOMBA aliko panga katika kijiji cha Nyerere alipopekuliwa alikutwa na dawa za aina mbalimbali zenye nembo ya MSD, Drip 500mls chupa tisa ambazo haziruhusiwi kuuzwa, sindano na baadhi ya vifaa tiba vidhaniwavyo vilipatikana kwa njia isiyo halali.
       
Kamanda misime amesema baada ya kuhojiwa kwa mtuhumiwa huyo alikiri kutenda kosa hilo na kusema kuwa hana taaluma yoyote ya utabibu na elimu yake ni darasa la saba. Uchunguzi zaidi unaendelea na mtuhumiwa atafikishwa mahakamani.

Hata hivyo kamanda misime ametoa wito kwa wananchi kuwa makini na kuhakikisha wanatibiwa kwenye Zahanati, Vituo vya Afya na Hospitali zinazofahamika ili kuepuka madhara dhidi ya tiba bandia. Pia wawafichue madaktari feki ili waweze kuchukuliwa hatua za kisheria kwani unapotibiwa na mtu ambaye hana Utaalam kama Daktari mbali ya kuumwa kwanza hutapona na pili utapata madhara ambayo yanaweza kukuletea madhara ya kudumu na pengine kupoteza maisha.
       


KAMANDA WA POLISI MKOA WA DODOMA AKITOA MAELEZO JUU YA KUKAMATWA KWA WATUHUMIWA WALIOHUSIKA NA MAUAJI KATIKA KITUO CHA MAFUTA CHA STATE OIL



WATU WANNE MBARONI KWA KOSA LA MAUAJI KATIKA KITUO CHA MAFUTA CHA STATE OIL MKOANI DODOMA.


           Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma SACP- David Misime

Jeshi la Polisi Mkoani Dodoma linawashikilia watu wanne kwa kosa la mauaji ya watu wawili walinzi wa Kituo cha Mafuta cha State oil kilichopo eneo la Kisasa  Mkoani Dodoma.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi SACP-DAVID MISIME amesema mnamo tarehe 7/8/2015 alitoa taarifa ya tukio la mauaji ya walinzi wawili waliouwawa usiku wa kuamkia tarehe 04/08/2015 huko katika kituo cha mafuta cha State Oil eneo la Kisasa Manispaa ya Dodoma ambacho kipo katika hatua za mwisho za kukamilishwa kujengwa ambapo kuligundulika tukio la kusikitisha la kuuawa walinzi wawili kwa kupigwa na kitu kizito kichwani hadi kupoteza maisha. 

aidha kamanda misime amewataja walinzi   Waliokuwa wameuawa ni PAULO NDULUMA, miaka 57 na ALOYCE s/o PATSANGO mwenye miaka 47.

Kamanda MISIME ametoa wito kwa Wananchi watusaidie kwa yeyote mwenye taarifa za watu waliohusika kufanya tukio hili la kinyama watupatie taarifa.

Kamanda MISIME amesema kutokana na Uchguzi wa Kitaalam na taarifa za raia wema tumefanikiwa kuwakamata watuhumiwa wanne waliohusika katika tukio hilo la mauaji ambao ni:-

1.   MENROOF JANUARI HAULE @ MINOFU, miaka 35, fundi ujenzi ambaye alikuwa katika kituo hicho cha State Oil na mkazi wa Nzuguni Dodoma.
2.   MUSTAFA SALUM RAJABU @ BABU, miaka 52, mfanyabiashara na mkazi wa Nzuguni Dodoma.
3.   EZEKIEL ANYELWISYE BAJILE @ EZE, miaka 40, dereva wa daladala na mkazi wa Nzuguni Dodoma.
4.   FRANK ERNEST DABAGA, miaka 24, utingo wa daladala mkazi wa Ihumwa Dodoma.  

Kamanda MISIME amefafanua kuwa mtuhumiwa wa kwanza alikuwa fundi ujenzi na mfanyakazi wa Kituo hicho cha State oil ambaye alikula njama na hao watuhumiwa watatu na  kuwavizia walinzi hao kisha kuwapiga kichwani kwa kutumia sururu na kuvunja container na kuiba mifuko 72 ya Sementi na fedha taslim za manunuzi ya vifaa vya ujenzi kiasi cha Tsh. 10,000,000/=. Baada ya kuiba walipakia katika gari lenye namba za usajili T. 169 AYR Toyota Hiace inayofanya safari zake kati ya Ihumwa na Dodoma mjini ambayo inashikiliwa kama kielelezo. Sementi hiyo walikwenda kuhifadhi dukani kwa MUSTAFA SALUM RAJABU huko Nzuguni ambapo ana duka la vifaa vya ujenzi.

Pia amesema mifuko 13 ya sementi imepatikana inauzwa dukani kwa MUSTAFA SALUM RAJABU. Pia sururu iliyotumika kwenye mauaji imepatikana ikiwa imetumbukizwa chooni katika  eneo la tukio ikiwa na michizi ya damu, baada ya watuhumiwa kuonyesha.

Kamanda MISIME ametoa wito  kwa jamii hasa wale wanaojihusisha na uhalifu watambue kuwa uhalifu haulipi kwani mwisho wake ni kukamatwa na kuishia kufungwa, pia wajiepushe na tamaa ya kujipatia mali kwa njia za mkato zisizo halali. Pia ni vizuri kutambua huwezi kuwa mhalifu hasa katika mkoa wa Dodoma usikamatwe inaweza kuchukua muda tu lakini lazima tutakukamata. Upelelezi ukikamilika watafikishwa mahakamani.

Ametoa shukrani za dhati kwa wale wote walioshirikiana na Jeshi la Polisi katika harakati za kuwatafuta wahalifu hawa naomba pia waendelee kushirikiana na Jeshi la Polisi kufichua wahalifu.

WATU WAWILI WAMEUAWA KIKATILI KATIKA KITUO CHA MAFUTA CHA STATE OIL MKOANI DODOMA.



WATU WAWILI WAMEUAWA KIKATILI KATIKA KITUO CHA MAFUTA CHA STATE OIL MKOANI DODOMA.



            kituo cha mafuta cha State Oil ambapo tukio hilo lilitokea




         Jeshi la Polisi Mkoani Dodoma mara baada ya kufika katika eneo la tukio


                  Kituo cha State Oil kilichopo Kisasa kikiwa bado hakijamilika

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi  SACP- DAVID MISIME amesema mnamo tarehe 04.08.2015 majira ya saa 07:30  katika kituo cha mafuata cha State Oil eneo la Kisasa  ambacho kipo katika hatua za mwisho za kukamilishwa kujengwa kulitokea tukio baya na la kusikitisha la kuuawa walinzi wawili kwa kupigwa na kitu kizito kichwani hadi kuuwawa.

Kamanda MISIME amesema kulingana na uchunguzi wa kitaalam umeonyesha wauaji hao walifanya tukio hilo usiku wa kuamkia tarehe 04.08.2015 lengo lao likiwa ni kuiba vifaa ambavyo vilikuwa vimehifadhiwa kwenye kontena, kwani baada ya kuwaua walinzi hao walivunja kontena na kuiba mifuko ya sementi 72 pamoja na fedha taslim kiasi cha 10,000,000/= ambazo zilikuwa za kulipa vibarua na kununua vifaa vya kukamilisha kituo hicho ambacho kinatarajiwa kuanza kazi siku za karibuni.

Kamda MISIME amesema walinzi waliouawa katika tukio hilo wamefahamika kwa majina ya PAULO S/O NDULUMA, MMASAI, MIAKA 57 na ALOYCE S/O PATSANGO, MMASAI, MIAKA 47 wote Wakazi wa Kisasa.

Ametoa wito kwa Wananchi wasaidiane na Jeshi la Polisi kwa yeyote mwenye taarifa za watu waliohusika kufanya tukio hili la kinyama watupatie taarifa. Pia wasikubali kununua sementi ambayo haina risiti ya duka linalofahamika na anayeona mtu anayeuza sementi ambayo anaona mtu huyo hana duka wala kiwanda cha sementi atoe taarifa kwa Jeshi la Polisi.

Vilevile amesema kwa yeyote ambaye kuanzia tarehe 04.08.2015 sementi imehifadhiwa katika eneo lake na inatia mashaka juu ya upatikanaji wake atoe taarifa ili kuepuka kuhusishwa na tukio hilo.

Aidha Kamanda MISIME amesema Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma litatoa zawadi ya Sh. 5,000,000= kwa yeyote atakayetoa taarifa za kuwezesha kukamatwa watu waliopanga na kushiriki kufanya tukio hilo la kinyama.

Pia amesema ni vizuri jamii hasa wale wanaojihusisha na uhalifu watambue kuwa uhalifu haulipi kwani mwisho wake ni kukamatwa na kuishia kufungwa.