Pages

Sunday, 25 August 2013

KOCHA WA DUNIA MUUMINI MARA BAADA YA KUKOSWA NA KISU NA PANGA AMEFUNGUKA

Muumini mwinjuma ambae alikuwa raisi wa victiria sound amefunguka na kusema juu ya mambo yaliyo jili baina yake na waziri sonyo
mwishi wa wiki hii kuna ugomvi mkubwa ulizuka bain aya raisi wa victoria sound muumini mwinju ma na mkongwe mwenzake wa musiki ambae pia nae ni kiongozi wa band ya victoria sound waziri sonyo
prince muumini mwinjuma amesema chanzo cha ugomvi wake na waziri sonyo ni kutokana na sms walizkuw awakitumiana muumini alimkataza waziri sonyo kuja amelewa kisha kupanda jukwaani waziri sonyo hakuwa tayarikwa hilo badala yake alilazimisha kupanda

siku iliyofuata sonyo alikuja na panga akawa anamtafuta mwinjuma na kumkosa kuku akisema ni lazima amuonshe lakini siku iliyo fuata mwinjuma alimtumia sms na kumwambia kuwa anatakiwa kuwahi mazoezi ndipo alikasirika na kumtukana matusi makubwa yasiyoelezeka na alikuwa akimtukani kwa mama yake mara baada ya hapi sonyo alikuja katika mazoezi na kumwambia mwinjuuma kwanini umenitukana smuumini akamwambia wewe ndie umeanza ndipo sonyo alichomoa kisu na kutaka kumchoma baada ya hapo mwinjuma akawa amekipangua kisu na kumpa ngumi sonyo hapo ndipo wakaja kuamuliwa na wanamuziki wenzao baada ya hapo mwinjuma aliondoka na kumchukulia RB baada ya hapo akapelekwa mahabusu

NDANDA COSSOVO AMESEMA LYVA KAONDOKA KATIKA BAND YA DIAMOND SOUND ORIGINA KUTOKANA NA UOGA WAKE


Mwi wa band ya diamond musica original  Ndandason Onawembo Cossovo ambae alikuwa ni mwimbjai wa band ya  Fm academia na stono musica na hatimaye kuanzisha band yake ya watoto wa tembo amesema yeye kuwa kiongozi wa band ya diamond musica sio kwamba ndie kawa raisi wa band hiyo

Ndanda Cossovo ambae amekuwa ni miogoni kwa waimbaji maarufu nchini Ttanzania kutokea nchini Congo kwasasa amekuwa kama mtu anaefundisha band ya diamond musica original,
Cossovo amesem  hayo mara baada ya ujio wake katika band ya diamond musica origina na kupelekea kusababisha kuacha kufanya kazi kwa raisi wa band hiyo Lyva sultani cossovo amesema  ameondoaka kwa kugombana na boss wake kutokana na kuhujumu mali nyingi za band hivyo asisingizie kuwa cossovo ndie chanzo cha yeye kung'oka katika band ya diamond sound original
 


Ndanda amesema huenda lyva anamuogopa kutokana na kazi ambazo anazifanya ,pia Cossovo amesema huenda Lyva amechanganyikiwa na Lyva amemuogopa kwani hamuwezi kwa kila kitu kuanzia uimbaji,umri,uzoefu wa muziki na yeye anamiliki band yake

Ndanda amesema yeye yupo katika band hiyo ni kwa muda mfupi na ni kwa ajili ya kufundisha na kuwapatia uzoefu wanamuzili wa band hiyo kutokana na uzoefu aliokuwa nao pamoja na kufundisha dawati la uongozi kwa ujumla kwani yeye bado anaendelea na band yake ya watoto watembo

Cossovo amesema kwa sasa anamkataba na  kampuni ya primus ambapo kwa sasa anafanya nayo kazi kutokanana hayo hana haja ya kukaa katika band ya diamond ikiwa nae ana band yake mwenyewe,kwa sasa Cossovo ameshakamilisha nyimbo yake akiwa ameshirikiana na mwanamuziki wa musiki wa dance nchini congo drc jb mpiana

COSSOVO AMESEMA ALIPOKUWA AKIZUNGUMZA NA SAFU HII QJ AFRICA MOTO kuwa kwa sasa band ya diamond sound original imejipanga vyema kwa mazoezi

MWIMBAJIWA MUZIKI WA DANCE NCHINI CHARLES BABA AMEAMUA KUACHANA NA UBACHERA

Charles baba ambae ni mwimbaji na ni raisi wa band  ya mashujaa musica band ameamua kufunga ndoa jana jumamosi katika kanisa la Mt Petro jijini Dar es salaam
Charles Baba ameamua kuoa na kuachana na mambo ya ukapela kwa sasa amepata kifaa kipya zaidi  ambacho ndicho chaguo lake katika maisha yake yote ameamua kufunga nae pingu za maisha ,Chrles Baba amesema  huyu ndie chaguo langu ambae nimeamua kula nae kiapo kanisani kwani ni jambo la kumshukuru mungu 
CHARLES BABA NA REHEMA SOSPETER
Charles Gabriel Cyprian amemuoa Rehema sospeter marwa murimi mtoto wa kikurya  jumamosi hii ambapo walifunga ndoa katika kanisa la  Parokia ya Mt Petro Oysterbay jijini Dar es Salaam  kuwa ndie muke wake wa ndoa
PONGEZI ZA DHATI PRESIDENT KUTOKA KWA SAFU YA QUEEN JOZZEE  MAMA AFRICA MOTO na wadau wote wa music wa dance



Thursday, 8 August 2013

ROGGERT KATAPILA MWANZO WA MUZIKI MPAKA SASA



                   
ROGERT HEGGA alizaliwa mwaka 1973 jijini Dar-es-salaam na kusoma shule ya msingi mpaka  kumaliza na hatimaye alijunga na chuo cha ufundi Dar-salaam DAR TECH
   Rasmi rogert alijiingiza katika maswala yamuziki mnamo mwaka 1987 kwa kuimba kwaya kanisani,
 
baada ya hapo mwaka huo huo wa 1987 alijunga na band iliyoitwa SAFARI BAND mwenyewe anaiita band ya mtaani wakati huo katika band alikuwa na mchekeshaji maarufu katika tasnia ya uigizaji Kingwendu ambapo alidumu na band hiyo ya safari mpaka mwaka 1989 ambapo alijunga na band nyingine iliyokua inajulikana kama City Sound ambapo alikutana na mkongwe wa muziki wa kiafrica toka Africa ya kusini TABOO 
 Baaday hapo mwaka 1992 alijiunga na band  iliyoanzishwa mwishoni mwa miaka ya tisini na kina kamarade Ally Choki band ya BANTU GROUP lakini wakati Roggert anajiunga na band hiyo ya bantu group tayari inaesemekana kuwa yeye pia ni muasisi wa band ya bantu group KOMANDOO HAMZA KALALA ndio alikua amejiunga na band hiyo ambayo roggert alidumu nayo mpka mwaka 1995
       Mnamo mwaka  1995 Rggert alifanikiwa kutoa album yake mwenyewe kama solo artist huku akiwa na kundi lake dogo la Africa generation wakati huo akiwa ametokea nchini Zimbabwe ambako alikwenda kufanya kazi  ya muziki wa dansi
 album hiyo ambayo aliipa jina la Mama Radhia ambapo ni moja ya kibao ambacho kilimtambulisha vilivyo rogert hegga nyimbo nyingine zilizopatikana katika album hiyo ni ASMA,SINTO KATA TAMAA,THEO MAZIMBABWE,
        Mwaka 1997 roggert alijiunga na band ya MASAI BAND ambayo ilikua na maskani yake pale kijitonyama jijini Dar es salaam kipindi hicho akiwa na waimbaji mbali mbali kama YAHAYA MKANGO,JOHN MPONI, ambapo hapo alidumu kwa muda wa mwaka mmoja tu na hatimaye
        Mwaka 1998 alijiunga na band ya Twiga Band iliyokua na maskani yake mwananyamala ambapo hapo alikutana na mtu mmoja maarufu sana CHE MUDUNGWAO, pamoja na JOHN MPONI ambapo hakudumu sana.
  
                            
Mwaka 1999 alijiunga  na band ya AFRICAN STARS kabla haijapewa jina la TWANGA PEPETA
ambapo hapo Alikutana NA wanamuziki mbali mbali akiwemo LE GENERAL BANZA STONE,LUIZA MBUTU ,AMIGOLASI,YAHYA MKANGO,JOSEPH KANUTI,DEO MWANAMBILIMBI,MICHAEL LILOKO,BOB GAD WILLIUM,JESCA CHALS,MAREHEM ABUU SEMHANDO kipindi hicho ilikua ni HOTEL BAND ambayo ilikua ikipiga  BAHARI BEACH lakini walifanikiwa kutoa album moja ya KISA CHA MPEMBA ambapo ndani yake kulikuan nyimbo moja ambayo ni utunzi wake roggert FADHILA KWA WAZAZI NO. 01 hata hivyo hakumaliza mwaka na african star mwisho mwa
         Mwaka 1999 alitimkia nchini  NAIROBI-
KENYA katika band moja iliyojulikana kama BENGA INTERNATIONAL ambapo hapo alikutana na wanamuziki nguli kwa sasa kama MUUMINI MWINJUMA,RASHID SUMUNI,hakudumu sana katika band hiyo na baadae kutimkia katika mji wa KISUMU ambapo hapoa pia likutana na mtu kama kamarade ALLY CHOKI ambae alikua kiongozi kwenye Band iliyoitwa EXTRA KIMWA ambapo hapo vile vile kulikupwepo na mpiga gita maarufu tanzania kwa sasa EPHRAIM JOSHUA  NA MTOTO  WA KING MAJUTO ATHUMAN MAJUTO, ambapo hapo alikaa kwa muda kidogo na baandae kurejea tena tanzania,
              mwanzoni mwa mwaka 2000 alitua tena AFRICA STAR ambapo aliikuta album ya pili ya twanga pepeta JIRANI ikiwa jikoni na yeye kuweza kupata kushiriki katika kuimba katika nyimbo zilizokuwemo katika album hiyo ambayo ilatakiwa kuitwa AUNGURUMAPO SIMBA lakini kabla haijamalizika kiongozi wa wakati huo banza stone aliondoka na ndipo ali choki alipewa jukumu la kuandika nyimbo itakayobeba jina la album 
                 Safari ya roggert haikuishia hapo mwaka huo huo wa 20000 mwishoni alijitoa yeye na wenzake na kwenda kuanzisha band ya MCHINGA SOUND ambapo alikutana na wenzake kina ADOLPH MBINGA,MWIJUMA MUUMIN,JOSEPH WATUGURU,MOSHI MSELELA,GODFREY KANUTI,MICHAEL LILOKO,SELEMAN BONGO hapo hakudumu sana katikati ya mwaka 2001 akajiunga tena african stars ambapo alidumu sasa kwa muda na kuweza kutoa nao album za
 2001-fainali uzeeni 2002-chuki binafsi-ambapo alitunga nyimbo ya La mgambo 2003-ukubwa jiwe-2004 mtu pesa ambapo ndani ya album hiyo alitunga nyimbo ya family confilc
          
mwaka 2010 alirudi tena Twanga pepeta na sasa ivi inaitwa Twanga oepeta internasional  ambapo hapo ailifanikiwa kutoa albm moja ambayo inaitwa mwana dar es salaam ambapo ndani kuna nyimbo ya rafiki adui ambayo ni utunzi wake mwenyewe roggert
     Mnamo  mwaka 2011 alihamia band yenye wanamuziki nguli wa siku nyingi na inayofanya vizuri katika tasnia ya muziki wa dansi ambayo ipo chini ya mkurugenzi mtendaji ally choki EXTRA BONGO NEXT LEVEL a.k.a WAZEE WA KIZIGO ambapo hapo ametunga nyibma ya UFISADI WA MAPENZI ambao utakuwepo kwenye album ambayo bado haijapewa jina na yeye yupo kama kiongozi wa band na hapo anaunga na wanamuziki LE GENERAL BANZA STONE,RAMA PENTAGONE,ATANASI,ALLY CHOKI MWENYEWE,SUPER NYAMWELA, AISHA MADINDA
  
Lakini kwa sasa roggert ameamua kuachana na musiki amesema anapumzika mara baada ya kufanya kwa muda mrefu na matarajio yake hasa kwa sasa ni fungus band yake mwenye hivyo hayupo band yeyote

Tuesday, 6 August 2013

MJUE MWIMBAJI WA BILNGE MUSICA NA KAZI YA MUSIKI

Huyu ni mwanamuziki kutoka band ya Bilenge musica du congo makazi yake ikiwa ni Nairob Kenya
anaitwa Bizo Chante amezaliwa Bukavu mashariki mwa jamhuri ya kidemocrasia ya watu wa congo mnamo 5 /11/1978.
Chante ni mtoto wa tano kutoka katika familia ya watoto saba,  mnamo tarehe 13 alijiunga kozi ya musiki kitumaini ya bukavu akiwa kama muimbaji wa kundi moja la kwaya katika chuo hicho
baada ya hapo alitimukia Quartie baghdad  kimuzikina akajiung ana band ya traction musica huku akiendelea kujifunza maswala ya music ambapo alikuwa ni musiki wa dini.
Mnamo mwaka 1999 Chante alitimkia nchini tanzania na kujiunga na Magnum Musica ,mwaka 2000 klirejea Nchini Nairobi Kenya katika banda ya Senza musica mpaka mwaka 2009-2011
baada ya hapo alielekea katoka band ya Limpopo kwa Mousa Djuma mwaka uleule wa 2011 ndipo alijiunga na band ya Bilenge musica,mwaka mmoja baadae bizo aliondoka kuelekea nchini Dubai alikaa kwa muda mfupi ndipo akareje tena nchini Kenya na kuendelea na band yake ya bilenge musica mpaka sasa bado anaitumikia band hiyo
Chante ni mpigaji wa drums za instrumental ni mwimbaji anapenda sana kuwa role  model wa music pia chante anamatarajio mengi katika band .

BAND YA MUSIC WA DANCE NCHINI KENYA MAARUFU KAMA BILENGE MUSICA KWA SASA WAMEKUJA KIVINGINE MARA BAADA YA KUZINDUA ALBUM MPYA

Bilenge musica ambao ni waimbaji wa musiki wa dance kutoka nchini Congo makazi yao yakiwa nchiniNairobi Kenya wamefanya uzinduzi wa album yao mpya ambayo inajulikana kwa la thermometre ambapo album hiyo imefanyiwa uzinduzi siku ya 13 july 2013
Bilenge musica ambao walifanya uzinduzi wa album hiyo katika ukumbi wa Village Dream South B siku ya jumamosi ambapo album hiyo ilimeonekana kuwa na nyimbo nzuri zaidi wameshukuru sana kwa mashabiki wao kuwapa saport kubwa

Bilenge musica band ambayo inawaimbaji mahili na wamewahi kuimba nyimbo kama vile malo malo,im transiferred.kiduani,miss kenya,musamaria na nyingine kibao wamesema album hii pia ni nzuri watu watengemee nyimbo nzuri kama za awali

bilenge musica ambao inawaimbaji kama Barzee Kalend ,Bizo Chante.Zaget de Longueur ,Benisoit Jack Assanik na wengine wengi kutoka nchini Congo wameshaiiiiachia album hiyo

Monday, 5 August 2013

LUCIEN BOKOLO MBIONI KUKAMILISHA ALBUM YAKE MPYA HIVI KARIBUNI


mwimbaji wa music wa dance duniani Lucien Bokilo ambae ni mwimbaji wa mtindo mbalimbali kwa sasa yuko mbioni kukamilisha album yake ambayo itakuwa na nyimbo za kutishia zilizoimwa kwa mahadhi mbalimbali

Bokilo ambae amewahi kuimba na kundi la soukous stars na alikuwa akiimba nyimbo za mtindo wa soukous ambao asili yake ikiwa ni congo kinshasa na congo brazzaville ambapo mziki huu ulianza pale 1930 amesema japo bado yupo na kundi hilo  lakini anafanya kazi za kujitegemea kama solo artist

Bokilo ambae ameimba na wanamuziki mbalimbali kama lokasa ya mbongo na wengine wengi na kutamba na nyimbo zake mahili duniani kama vile one way,missete,aicro de toi,aziza,djoukende,mwasi,ngoma,retuorne toi,robin na nyingine nyingi,Bokilo amesema kutokana na shoo ambayo wanayo ya kwenda canada akiwa na kundi zima la soukous stars akirejea ataendelea na kazi zake za kumalizia album yake studio